Sasa hivi mtoto mwenye umri mdogo mno anaweza kuwa milionea huku wewe uking’ang’ana kwa kuwekeza hapa na pale. Walimu wa kingereza na Kiswahili hujitolea kwa jino na ukucha kuwasukuma wanafunzi kuandika insha aghalabu ukurasa mmoja na nusu. Kunao ambao husimulia kisa kwa ubunifu wa aina yake, na kunao ambao hushindwa kabisa kubuni kisa. iwapo insha inahusu safari ya ughaibuni, utawasikia wengine wakisema eti ‘mimi sijawai kuwa ughaibuni! Nitaandika nini? Hata hivyo, baada ya mwalimu kuorodhesha vidokezo, kuna wale ambao hujieleza kwa ufasaha na ustadi wa aina yake. Hivyo ndivyo watoto hawa wanaotawala mitandaoni kama vile: Tiktok, youtube, facebook na hata instagram wanafanyiwa. Japo wengine huzaliwa na ubunifu wa ziada, mwongozo wanaopewa huwasaidia mno. Watu wengine huwa mbioni kuiba ubunifu wa wengine na kuukimbiza jikoni ili upikwe uive kabla ya mumiliki halisi kuanza kuutumia. si mara moja umeona watu wakiweka video zenye maudhui ya aina yake bila hata kuwatambua walioyabuni maudhui hayo. Ni wao ndio huishia kupata ‘donge’ nono huku mumiliki akibaki kuwa hohehahe! Lakini haya yote yanaweza kuzuilika kivipi? Enda katika DUKA LA MAARIFA hapa www.radioibukalive.com ujinyakulie nakala ya: ‘MAHALI PA KUUTUMIA UBUNIFU WAKO KAMA MNYONGE ILI USIIBWE NA ‘WALIO NAVYO’ NA KUKIMBIZWA JIKONI KABLA YA WEWE KUPATA KIBERITI’
Summary
Article Name
MAKALA
Description
Wengi wanapoona mtu akifaulu kwa kufanya kitu fulani wao hujaribu kuiga ili wawe kama YEYE. Kuna athari gani ya kukosa ubunifu wako?
Author
Ibuka Fm
Publisher Name
www.radioibukalive.com
Publisher Logo