Iwapo utamuuliza yeyote kuhusu safari yake ya kimaisha huenda akasita! Asikupe jibu la moja kwa moja labda kutokana na pandashuka alizozipitia au matatizo anayoyapitia. Hata wengine huzidiwa na hisia na kuanza kulia. Katika makala ya ‘STORI’ yangu na kituo cha redio cha Ibuka fm, Rita Amalemba { Mzaliwa wa maeneo ya magharibi ya Kenya alisimulia ‘stori’ yake japo kwa kiduchu! Kulingana naye, anasisitiza kuwa hali ya binadamu kuwa na sura mbili si porojo tu bali ni ukweli mtupu. Anasema kuwa sura moja huwa ni ya ‘Umaskini’ Shida, na mahangaiko ilhali nyingine huwa ni ya ‘Utajiri’ raha na starehe. Rita aliongezea kwa kusema kuwa japo kuna wale ambao huzaliwa tu na kuvishwa sura ya utajiri, wale wasiojituma na kuwajibikia urathi na urithi huo huishia kuionja sura hiyo ya umaskini au kuwachia kizazi cha nyuma kwa kufuja mali yote. Japo hajigambi kwa ufanisi alio nao, anawahimiza watu waikumbatie bidii na kuiaminia safari na hatua za kimaisha alivyopanga mwenyezi Mungu.

UNAKUBALIANA NAYE?

Summary
'STORI' YANGU
Article Name
'STORI' YANGU
Description
Kuna watu ambao ukiwauliza kuhusu safari ya maisha yao wao huangua kilio. Ni mambo yapi haya ambayo huwajia akilini na kuwahuzunisha kiasi hicho? Katika makala ya 'STORI' yangu, wengi wanaunguka na kujieleza.
Author
Publisher Name
Ibuka FM
Publisher Logo
Tags:

Leave a Reply