Chanjo za ugonjwa hatari wa Mpox zinatarajiwa kuwasili katika bara la Afrika hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa, chanjo hizo zimepatikana katika sehemu nyingine za dunia. Awali, dozi 10,000 zilitolewa na Marekani na zitatumika kukabiliana na aina mpya ya virusi hivyo. Hadi sasa, kuna mataifa ambayo yameathirika na serikali imewahimiza wahasiriwa kufwata mwongozo wanaopewa na maafisa wa aya ili kuzuia uenezaji na maabukizi zaidi. Mpox ambao hapo awali ulijulikana kama monkeypox, ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi aina ya orthopoxvirus. Ugonjwa huu umekuwa tishio hasa katika jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na nchi zingine. Dalili za kawaida za Mpox ni upele wa ngozi, ikifwatana na homa kali, maumivu ya kichwa, misuli na mgongo Ugonjwa huu unaweza kuambukizwa kwa kugusana. Zidi kufwatilia tovuti yetu ya www.radioibukalive.com kwa habari ibuka.
Summary
Article Name
CHANJO YA MPOX
Description
Mahangaiko ambayo bara la Afrika limeyashuhudia kutokana na mlipuko wa gonjwa hatari la Mpox huenda yakafikia kikomo hivi karibuni baada ya chanjo kugunduliwa.
Author
Daudi Wa Nyongesa { Mhariri Mkuu Ibuka FM}
Publisher Name
Ibuka FM
Publisher Logo