Mikasa ya moto limekuwa donda dugu hasa kwa wafanyibiashara wadogo wadogo ambao hujikakamua ili kukusanya mtaji wa kuazisha biashara zao. Wengi wao kutokana na pato lao la chini, hushindwa kuwatafuta watu waliohitimu ili kuwakarabatia nyaya za stima katika eneo wanalofanyia biashara. Kule Kaburu; Lancas katika kaunti ya Uasin Gishu, jamaa mmoja alipigwa na butwaa baada ya kupata habari kuwa kibanda alichokitegemea kumlisha na kumvisha kimemumunywa na ndimi za moto ambao unakisiwa kusababishwa na hitilafu za nguvu za umeme. Mkuu wa Polisi katika eneo hilo amewahimiza wenyeji kuwatafuta watu waliohitimu wanapotaka kuunganishiwa nyaya za stima ili kuepuka visa kama hivyo. Wakati wa tukio hilo, hakuna yeyote aliyepata majeraha wala kupoteza maisha. Duru za kuaminika zinadokeza kuwa mumiliki wa kibanda hicho alizirai kabla ya kurejesha fahamu baadaye. Kwa habari zaidi, zidi kuwatilia tovuti yetu ya http://www.radioibukalive.comwww.radioibukalive.com
Summary
Article Name
HASARA YA MOTO KWA 'HASOLA'
Description
Aliinama tu chini na kuzirai alipopata habari kuwa kibanda chake cha 'Chips'Kimeteketea kwa moto wa stima.
Author
Daudi Wa Nyongesa {Mhariri Mkuu} Ibuka FM
Publisher Name
Ibuka FM
Publisher Logo