DARASANI / DINI / MAHUSIANO / MAKALA / MALEZI / MJADALA / SIASA / SIMULIZI / SPOTI / USHUHUDA / VIPAJI VYETU / YANAYOJIRI September 6, 2024
Japo vipo vituo vingi vya redio duniani, Ibuka FM ni kituo cha redio ambacho kauli mbiu yake ni ya kipekee. Ni redio ambayo malengo yake si ufwasi tu bali kuelimisha na kuwafungua macho wapenzi wasikilizaji na wasomaji wa makala kwenye tovuti yake ya www.radioibukalive.com. Miongoni mwa mashabiki hawa shakiki, wanafunzi wamepewa kipaumbele kwani ni hapa ambapo watafunuliwa ukweli kuhusu thamani ya vipaji/talanta zao katika kujiimarisha kimaisha. Mambo yanayoangaziwa kwa kina na kituo hiki pamoja na tovuti yake ni masuala ibuka al maarufu masuala mtambuko katika mtalaa wa Umilisi { C.B.C}. Haya ni mambo ambayo ni muhimu sana kwa wanafunzi na hata umma kwa jumla. Si mara moja umekutana na mtu barabarani kisha ukamuuliza kile kinachoendelea katika taifa, mtaa wake au hata duniani naye akakosa mwao kabisa! Lakini masuala ibuka ni yapi hasa? Haya ni mambo ambayo hutokea kila kuchao! Kuna yale mambo ambayo yanaweza kutokea kwa ghafla mahali fulani na yakasahaulika hata kabla jua kutua! Na kuna masuala makuu ambayo hubaki kuwa gumzo vinywani mwa watu kwa muda ulani. Yote hayo ni masuala ibuka ila tofauti ni muda wa kudumu. Mifano ya mambo haya ni kama ipi hasa? Kuna mifano mbalimbali ya masuala ibuka ambayo hulikumba taifa au eneo fulani la dunia. Mathalan: Mafuriko, Njaa, Ukame{ Kiangazi}, magonjwa, umaskini, ufisadi, ugaidi, ukosefu wa usalama , ajali, miongoni mwa mengine. Na je, masuala ibuka ni sharti yawe mambo mabaya pekee? La hasha, tukio linaweza kuwa zuri au baya. Ni vile matukio mengi huwa hayapewi mwangaza sana hivyo kuzungumziwa na watu wengi huwa muhali mno. Kwa mfano kuna masuala ibuka chanya amabyo yaweza kulenga sekta kama vile: Mazingira{Tabia nchi}, Haki za wanyama na binadamu, Elimu, Talanta na michezo, Utalii, Usafiri, Teknolojia { Kwa mfano kunawezakuwa na uzinduzi wa kifaa kipya ambacho kitazua gumzo kote kote!} miongoni mwa mengine mengi. Halikadhalika, tovuti hii inawapa wanafunzi hasa wanaouendeleza mtalaa wa C.B.C ufahamu wa mawazo na miradi ambayo inaweza wafaidi katika umri wao mdogo ili akiba yao iwe nono katika maisha yao ya halafu. Kila siku, usikose kuingia katika tovuti yetu ya www.radioibukalive.com
Fanya hivi: Jiunge na ‘Mail List’ yetu ili uwe wa kwanza kupashwa yanayojiri. Pia, kuwa miongoni mwa wale ambao wapo katika Channeli yetu ya Whatsapp. Tumia kiunga hiki kujiunga https://whatsapp.com/channel/0029Vao1Tcx6hENy2LIBWa0h