Tangu jadi, tovuti nyingi ambazo zimekuwepo zimekuwa zikiangazia masuala ya watu maarufu ‘aka’ Celebrities, porojo za siasa pamoja na mambo mengine ya kutisha tu. Ni dhahiri kuwa wanafunzi wamekuwa na upweke na wakati mwingine kujikuta pia wanayasoma tu mambo hayo, waangue kicheko au kilio, si hoja kwa mwandishi. Wengi wa wanafunzi hawa wamekuwa na kiu ya kukuza ubunifu wao kwa njia moja au nyingine. Uzinduzi wa kituo kipya cha Ibuka FM na tovuti ya www.radioibukalive.com umewapa wanafunzi hawa afueni. Wenyewe sasa wanaweza kuingia kwenye tovuti hiyo na kusakura matini yenye umuhimu kwao. Pia wanaweza kujinoa makali kwa kuchangia katika makala na mijadala inayochapishwa katika tovuti hiyo. Daudi wa Nyongesa { mmoja wa wahariri katika kituo hicho} alisema kuwa watoto huiga wanachokiona. Aliongezea kwa kusema kuwa japo watoto wengi wamenunuliwa simu, vipakatalishi pamoja na tarakilishi na wazazi wao, bado hawajakuwa wakivitumia kwa njia inayofaa. Wengi wamekuwa wakishinda kwenye simu zao kutwa nzima kubovya na kutazama video zenye aibu na kuangua vicheko vya kudondoza machozi. Hata kuna wale ambao hawalali usingizi wa kutosha kutokana na uraibu huu usiolipa wala kufaidi. Aliongezea kuwa tovuti kama www.radioibukalive.com itamsaidia mtoto kutojishughulisha na mambo hatari ya mitandaoni kama vile: Kushiriki michezo ya kamari, kutazama filamu hatari kama za ngono na ujambazi. Daudi alisema kuwa katika tovuti hiyo bado kuna matini ambayo mwanafunzi anaweza kununuliwa na mzazi wake ili yamsaidie kupanuka kimawazo. Halima ambaye pia ni mwanahabari katika kituo hicho alisema kuwa kwa sasa, kuna mtoto ambaye hajafikisha hata miaka kumi na miwili! Ni mwanafunzi na amewaajiri hadi walimu wake kazi. Ibuka FM inaamini kuwa katika siku zijazo, wanafunzi watakuwa wanayakamilisha masomo yao huku wakiwa na ubunifu utakaowafaa na kuwasaidia kujitegemea na kujiajiri mitandaoni. Na kwamba umefika wakati ambapo muda anaotumia mtu mtandaoni iwapo haumlipi wala kumfaidi kivyovyote, basi ajiite mkutano!
50 IDEAS IN C.B.C THAT MAY PAY THEIR SCHOOL FEES