Tangu kuzinduliwa kwa tovuti ya www.radioibukalive.com, Kituo hiki cha redio kinaendelea kupata umaarufu na wingi wa ufwasi hasa kutokana na vipindi na makala yake ya kipekee. Katika tovuti ya kituo hiki cha redio, uratibu wa makala na vipindi umelenga masuala ibuka. Yaani mambo ambayo wanajamii wanakumbana nayo kila siku. Kwa mfano, wengi wameipenda sehemu ya ‘SIMULIZI’ ambapo watu hasa wale ambao wamebaleghe hupewa nafasi ya kusimulia chimbuko au asili ya kitu, jambo au hata majina wanayopewa pindi wanapozaliwa. Japo si wote ambao huwauliza wazazi asili ya jina lao, simulizi za wengi ni za kutamausha na kuhuzunisha. Abubakar Omar { Shabiki sugu wa redio kutoka Watamu} aliiandikia Ibuka fm na kusema kuwa yeye kila anapoamka asubuhi baaday ya kusali, lazima atembelee tovuti ya www.radioibukalive.com ili kufwatilia simulizi zilizochapishwa pamoja na masuala yanayojiri. Je, una simulizi lako ambalo ungependa tukusikilize na tuchapishe? Wasiliana nasi sasa!

Leave a Reply